ASKARI POLISI AUAWA NA GARI KUCHOMWA MOTO KIBITI

Posted on

Watu wasiojulikana wamemuua kwa kwa kimpiga risasi Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama barabarani na kisha kuchoma moto gari alilokuwa analitumia.
Tukio hilo limetokea leo mchana katika Kijiji cha Bungu B wilayani Kibiti Mkoani Pwani ambapo vikosi vya usalama vilianza safari wakati huo kwenda eneo la tukio.
Jeshi la Polisi halijatoa taarifa yoyote hadi sasa kuhusu tukio hilo.
Tukio hili limetokea ikiwa ni saa chache tangu Rais Magufuli aliposema kwenye mkutano wa hadhara Mjini Kibaha kuwa wahalifu hao katika Wilaya za Kibiti na Rufiji wameanza kushungulikiwa na moto wameupata.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tR5nVD
via IFTTT

MESSI AMSIFU CRISTIANO RONALDO

Posted on

Staa wa soka wa timu ya Barcelona, Lionel Messi amesema kwamba huwa anapenda jinsi mashabiki wa soka duniani pamoja na vyombo vya habari vinavyowalinganisha (Messi na Ronaldo). Ronaldo ametupia magoli 16 katika mechi 10 za mwisho ambapo Real Madrid waliweza kutwa taji la ubingwa wa ligi kuu wa Hispania (La Liga) kwa msimu wa pili mfululizo na kushinda kombe la ligi ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo pia.
“Hapana, mara zote nimekuwa nikisema hili, kwamba [Ronaldo] kwa upande wake – anang’ara zaidi kwa uwepo wetu sote,” kituo cha ESPN kilimkariri Messi as akiiambia Tencent.
“Sisi sote tunajituma ili tupate matokeo mazuri kwa timu zetu, na linalosemwa nje ya hayo sidhani kama ni muhimu sana. Ronaldo ni mchezaji bora mwenye kiwango cha juu sana,” amesema Messi.
“Dunia nzima inajua, na ndiyo sababu yeye ni miongoni mwa wachezaji bora kabisa duniani. Kila msimu mpya unapoanza, mchezaji unatakiwa kuwa bora kuliko msimu uliopita. Tunacheza ili tupate matokeo mazuri, tushinde mataji zaidi na kuingia kwenye fainali ya klabu bingwa Ulaya na pia kushinda ubingwa wa La Liga.”
“Mwaka huu haukuwa wetu. Tulijaribu kwa uwezo wetu wote, lakini ikashindikana; tukaishia kwenye kombe la Mfalme. Tunategemea msimu unaokuja utakuwa mzuri kwetu kwa maana ya kushinda mataji,” alimalizia Messi.

from Blogger http://ift.tt/2sTlyo6
via IFTTT

MFUNGWA AISHI KIFALME AKIENDELEZA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA GEREZANI

Posted on

Kamishna Sianga anasema vita dhidi ya usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya ni ngumu na hatari kuliko wengi wanavyoamini, na wakati mwingine wamejikuta wakihatarisha maisha yao.
“Tunapambana. Tunachofanya sasa ni kuhakikisha tunadhibiti na kuua kabisa mtandao wa waingizaji na wauzaji wa dawa za kulevya, na katika hili tunapata mafanikio makubwa,” anasema.
“Mpaka sasa tumewakamata mapapa 15 wanaojihusisha na uuzaji wa dawa hizo hapa nchini. Si kwamba tumefanikiwa kumaliza tatizo, lakini jamii inatakiwa kujua biashara hii ina mtandao mkubwa ni wa watu wenye pesa nyingi. Tumekamata hao 15 lakini kuna kundi jingine tena limeibuka.
“Yaani iko hivi, mkiwakamata hawa unaibuka mtandao mwingine. Kwa hiyo si kazi ndogo. Tunapambana sana kiasi kwamba tunatishiwa kuuawa.” Anasema wanaoendesha biashara hiyo ni watu wenye jeuri ya pesa.
“Nakumbuka wakati tunaenda kumkamata mmoja wa kigogo wa unga (alimtaja jina), alitaka kuonyesha jeuri ya pesa. Tulipofika kwake akawaambia vijana wake ‘wana njaa tu hao waulize wanataka shilingi ngapi?’,” anasema.
“Kinachoshangaza zaidi watu hawa wana mtandao ulioingia hadi ndani ya Serikali kwa maana kwamba wapo watu ndani ya Serikali wanafahamu shughuli zao na wanawalinda. Wengine ni wafadhili wakubwa ndani ya makanisa na kwenye jamii, wapo ambao ukitokea misiba kwenye jamii zao wao wanaubeba kwa kila kitu mpaka mazishi.
“Nilipomkamata muuzaji mmoja (anamtaja) baadhi ya viongozi wa dini na vigogo wa Serikali walianza kunipigia simu na wengine kunifuata ofisini wakilalamika kwa nini nimemkamata mfadhili wao na wengine wanakwenda mbali zaidi na kudai kuwa tumemuonea.”
Sianga anasema taarifa walizonazo muhusika mmoja wa dawa hizo ambaye alimtaja jina, alikuwa ni mfadhili mkubwa wa ofisi moja ya Serikali. Anasema mtu huyo alikuwa akigharimia matengenezo ya magari ya ofisi hiyo na kusomesha mpaka watoto wa watumishi wa Serikali. Anasema wakati mwingine hugharamia sherehe za harusi za watoto wa vigogo wanaomlinda na hata kuwalipia mahari.
Anasema kiongozi mmoja wa ofisi ya Serikali, ambaye alimtaja jina, alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakimlinda (muuzaji huyo) ili asikamatwe, hata juhudi za kumkamata zilipofanyika, alikuwa anavujisha siri.
Anasema muuzaji huyo wa dawa za kulevya, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha maisha gerezani, anaishi gerezani kama mfalme.
“Tunapata taarifa kutoka gerezani kuwa anahudumiwa vizuri na inavyosemekana huenda wakati mwingine halali hata gerezani,” anasema. Kamishna wa masuala ya sheria wa mamlaka hiyo, Edwin Kakolaki anasema yupo mtu aliyefungwa kwa biashara ya madawa lakini anaishi gerezani kama mfalme na anaendesha biashara yake kama kawaida.
“Mbaya zaidi akiwa gerezani alinunua nyumba na watu wakachukuliwa kwenda kukaa katika nyumba ile kwa kazi moja tu ya kumpikia chakula.
Anasema nyumba hiyo hutumika kupikia chakula asubuhi na mchana kwa ajili ya mfungwa huyo wa dawa za kulevya na wakati anapoumwa, mkuu wa gereza huagiza apelekwe hospitali ambako pia huhonga ili alazwe hata wiki tatu.
Chanzo: Mwananchi
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sWXH7S
via IFTTT

HII NDIO SABABU YA JAJI WA MAHAKAMA KUU, MWENDWA MALECELA KUAMUA KUJIUZULU

Posted on

IKIWA imepita mwezi mmoja tangu majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuacha kazi kwa wakati mmoja na kuibua mjadala, jaji mwingine amejiuzulu wadhifa huo.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi na Mawasiliano ya Rais Ikulu jana ilieleza kuwa Rais Dk. John Magufuli ameridhia ombi la Jaji wa Mahakama Kuu, Mwendwa Judith Malecela kujiuzulu wadhifa wake.
Majaji wengine waliojiuzulu ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Jaji Aloysius Mujulizi na mwenzake Upendo Msuya ambao ombi la kujiuzulu kwao liliridhiwa na Rais Magufuli Mei 16, mwaka huu.
Jaji Mujilizi alikubwa na tuhuma za kuhusishwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow kwa kupewa fedha, huku Jaji Upendo ikielezwa kuwa ni mgonjwa.
“Rais Magufuli ameridhia kujiuzulu kwa Mheshimiwa Mwendwa Judith Malecela kuanzia leo (Juni 20, 2017),” ilieleza taarifa hiyo ya Ikulu.
Chanzo kingine cha habari kililieleza MTANZANIA kuwa tangu alipoteuliwa mwaka 2010 na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, jaji huyo hajawahi kusikika wala katika shughuli zake za ujaji.
Taarifa hizo zilielezwa kuwa jaji huyo wakati wote alikuwa akisumbuliwa na maradhi hali iliyomfanya ashindwe kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa utaratibu.
“Tangu alipoteuliwa Jaji Mwendwa, amekuwa akisumbuliwa na maradhi hali iiliyokuwa ikimfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake. Nafikiri kwa hali hiyo ndiyo huenda ni sababu ya yeye kuamua kuomba kujiuzulu wadhifa wake,” alisema mtoa taarifa huyo.
Mbali na majaji hao Mei 16, mwaka huu pia Rais Magufuli aliridhia kuacha kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, huku kilichowafanya kuacha kazi kikiwa hakijaelezwa.
Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa siasa walihusisha kuomba kuacha kazi kwa Jaji Mujulizi, kuwa kunatokana na kashfa ya Escrow, wakisema amesoma alama za nyakati.
Jaji Mujulizi alikuwa ni mmoja wa vigogo waliotajwa kupokea mgawo wa Sh milioni 40.4 kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira, uliotokana na fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Jumla ya Sh bilioni 321 ziliwekwa katika akaunti hiyo na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kusubiri suluhu ya kesi yake na Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Siku chache baada ya kuibuliwa kwa kashfa hiyo, Rugemalira aliyekuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa za IPTL, alisema kati ya fedha zilizokuwa katika akaunti hiyo, alilipwa Dola za Marekani milioni 75 sawa na Sh bilioni 120 ambazo aliziita ‘vijipesa vya ugoro’.
MTANZANIA.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sWPgtf
via IFTTT

Diamond Platnumz Amkana Hamisa Mobeto

Posted on

Msanii wa muziki Diamond Platnumz amekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Hamisa Mobeto ana mimba yake.
Aidha muimbaji huyo amekanusha pia kuwahi kutoka kimapenzi na video queen huyo ambaye anatikisa katika tasnia ya urembo.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm Jumatano hii wakati akiutambulisha wimbo wake mpya ‘I Miss You’, Diamond amedai tetesi za yeye kutoka kimapenzi na Hamisa zilianza baada ya kufanya naye kazi katika project ya wimbo, Salome.
“Toka nimeshoot na Hamisa Mobeto wimbo wa Salome, watu wamekua wakituhusisha pamoja, ujauzito wa Hamisa sio wangu,” alisema Diamond. “Jamani mwenye mimba si ajitokeze, si unajua hata mtu wake atakuwa anajisikia vibaya,”
Pia muimbaji huyo amedai wasichana wengi ambao anafanya nao kazi upakaziwa kuwa anatoka nao kimapenzi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sXdlzU
via IFTTT

Maalim Seif Apata Pigo Kubwa zaidi Kutoka Kwa Lipumba, Bodi ya Lipumba Yasajiliwa na Ruzuku itakuwa yao

Posted on

Kambi ya Cuf ya Ibrahim Lipumba imethibitisha bodi yao kupata usajili mpya kutoka RITA na sasa bodi ya wadhamini ya zamani imefutwa
Kwa sasa miamala yote ikiwemo ruzuku itakuwa inaingia kwenye akaunti na watakuwa wanachukua upande wa Lipumba na kutokana na bodi hiyo kufutwa wamesema kesi zilizokuwa zimefunguliwa dhidi yao na bodiya zamani watahakikisha zimefutwa.
Upande wa maalim seif wamesema kwa sasa hawana cha kuzungumza hadi watakapokaa
RITA walipopigiwa simu hawakupokea.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2stlx9X
via IFTTT

Rais Magufuli: Hata Kama Ikulu Hawajalipa Bili ya Maji, Kateni

Posted on

Rais John Magufuli amesema taasisi yoyote ambayo haaitalipa bili za maji, hata kama ni Ikulu ikatiwe maji.
Aliyasema hayo jana Jumatano katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani na kusisitiza kuwa miradi ya maji na ulipaji wa bili za maji ni muhimu.
“Mtu asipolipa bili, iwe taasisi yoyote hata kama ni Ikulu, narudia kusema kata,” alisema na kuongeza:
“Kwa sababu tumezoa kudekezana, kwenye mawizara haya nafahamu, fedha za OC na hata fedha za bajeti wanazo, lakini suala la bili ya maji linakuwa si la lazima.”
Alisema unamkuta kiongozi ana faili la kwenda Ulaya, anaenda kwanza Ulaya, ana semina analipa kwanza semina maji anaona si lazima.
“Lakini pale hakuna maji, na wale hawajalipia bili, kwa hiyo fundisho la hapa ni kukata,” alisema.
Alisema hata kama ni hospitali wakatiwe kama hawajalipa kwa sababu wana bajeti.
Alisema kama Mkurugenzi wa wilaya yupo na maji yamekatwa, basi hafai kuwa mkurugenzi.
“ Tukifukuza wakurugenzi kama 10, 20 hivi wale wengine watawahi kwenda kulipa bili za maji,” alisema.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rUmCIW
via IFTTT