Month: February 2017

Maiti zazikwa Juu ya zingine jijini DSM

Posted on

Hali ya Jiji la Dar es Salaam katika kipindi hiki inakabiliwa na maeneo mengi ya makaburi kujaa, hasa ya katikati ya mji na yale yaliyo katika halmashauri za wilaya.
Likiwa na idadi ya watu milioni 4.36 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, linapokea watu wengi kutoka maeneo mengine kiasi cha kufanya wastani wa ongezeko la watu kuwa asilimia 5.6.
Katika baadhi ya maeneo maarufu ya Kisutu, Kinondoni, Sinza, Chang’ombe, Wailes, Buguruni na Ubungo, maiti zinazikwa juu ya zile zilizofukiwa awali.
Maeneo ya katikati ya jiji kama Kisutu na Kinondoni ndiyo yamekithiri kwa maiti kuzikwa juu ya nyingine, na hata ule utamaduni wa ndugu kushiriki kuchimba makaburi sasa unapotea kutokana na wachimbaji kuchelea kuruhusu watu wengine kushuhudia shughuli hiyo.
Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alipozungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, amesema maeneo ya makaburi maarufu kama Sinza Makaburini, Ubungo na Kibo yanayotegemewa na manispaa hiyo, yameshajaa.
“Ubungo pamoja na wakazi wake kuwa wengi, kuna sehemu tatu maarufu za kuzikia; Sinza, Ubungo Maziwa, Kibo na Kimara na zimeshajaa. Sasa huko kote inabidi tufunge na kutafuta maeneo mapya ya kufanya shughuli za mazishi isiwe kuzika marehemu juu ya marehemu,” amesema Jacob.
Chanzo: Mwananchi

from Blogger http://ift.tt/2kM3HYx
via IFTTT

Bangi yasababisha Polisi wanane kutimuliwa Kazi

Posted on

Baada ya Mahakama ya Kijeshi kuwatia hatiani polisi wanane mkoani Kilimanjaro kwa kukamata magunia 10 ya bangi na kuyaachia, wamefukuzwa kazi.
Tukio hilo la polisi kukamata bangi hiyo, lilitokea Oktoba mwaka jana likihusisha askari wa Kituo cha Polisi Sanyajuu wilayani Siha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kuchukua hatua hizo baada ya kuridhika na tuhuma dhidi yao.
“Ni kweli kama ulivyopata hizo taarifa. Nimechukua uamuzi huo baada ya kuthibitishwa walikamata magunia 10 ya bangi na kuyaachia. Yule mkaguzi suala lake tumelipeleka juu,” amesema.
Polisi waliofukuzwa kazi kwa fedheha ni Sajenti Sadick D.6004, Koplo Innocent (D.9830), Koplo Deusdedit (E.1703), Koplo Semu (E.7525), Koplo Salum (E.8907), PC Kiroga (F.8983), PC Filbert (F.8385) na PC Ramadhan (G.3222).

from Blogger http://ift.tt/2kAXW4U
via IFTTT

Mwanaume alazimika Kuishi na Maiti ya mama Yake Ndani

Posted on

Marehemu Bi Henderika Apondi Were (aliyeashiriwa pichani).
MWANAMUME amelazimika kuishi na jivu la maiti ya mamake baada ya kukosa nauli ya kusafirisha jivu hilo hadi kaunti ya Siaya nchini Kenya.
Kulingana na Samson Were, 25, Bi Henderika Apondi Were ambaye ni mamake mzazi aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 45 baada ya kugongwa na gari la moshi nchini Ujerumani Septemba 2016.
“Mama alikuwa amekatwakatwa na gari la moshi kwenye ajali hiyo nikasema achomwe manake alikuwa vipandevipande alipozolewa. Walihifadhi mabaki ya mwili wake na kusafirisha hadi humu nchini,” akasema.
Kijana huyo alisema aliandikiwa barua na rafiki ya mamake ili atie saini kwamba hatopigania wala kufuatilia mali ya mamake huko Ulaya; ingawa alikataa kutia saini barua hiyo iliyotumwa kieletroniki.
Mama huyo aliolewa na Mjerumani Stephan Gronert jijini Nairobi Julai 5, 1994.
Kulingana na mwanawe Bi Apondi, baada ya ndoa wawili hao walisafiri nchini Ujerumani baada ya wiki moja.
Mumewe alifariki baada ya kuhusika kwenye ajali mwaka 2011.
“Huyu baba naye aligongwa na treni akafa. Mamangu ananisumbua na ndoto anataka kuzikwa bara lakini sina namna, mama anataka kuzikwa kwa shamba lake huko Siaya. Nataka nimzike kwa shamba letu mahali nitajenga,” akasema.
Alisafirishwa nchini Februari 3, 2017.
Sanduku
Were alisema ananuia kununua sanduku la futi nne ambapo ataweka jivu la mamake.
“Nikishaweka jivu sandukuni nitaweka nguo nyeupe, Nitanunua nguo ambayo nitamzika nayo. Nitamzika kama vile mtu wa kawaida anafaa kuzikwa,”akasema.
Were ameitaka Wizara ya Maswala ya kigeni kuhakikisha inafuatilia kifo cha mamake.
“Mama alikuwa ameniambia atanitumia Sh10 milioni nianze kufanya biashara lakini kesho yake nikapigiwa simu na rafiki yake kuwa amegongwa na gari la moshi. Ninashuku sana kifo chake. Isitoshe tunataka serikali ifuatilie mali aliyoiacha manake sisi hatuna namba,” akasema Were.
Alisema wajomba zake walizika mgomba kama mila za Kijaluo Oktoba 2016 huko Samia, Busia.

from Blogger http://ift.tt/2lX9ZJM
via IFTTT

Akatwa Mkono Baada ya Kufumaniwa na Mke wa Mtu

Posted on

POLISI katika Kaunti ya Kisii nchini Kenya wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 40 alikatwa mkono katika kijiji cha Matongo, Kaunti ya Kisii kwa madai ya kula uroda na mke wa mtu.
Bw Richard Omoke aliyejeruhiwa, alipatikana akiwa amelala na mke wa mwanamume aliyemkata jikoni mwa mwanamke huyo. Mumewe mwanamke huyo alimshambulia kwa kutumia upanga na kuukata mkono wake hadi ukaanguka kando.
Mume huyo, Bw Vincent Gwaro mwenye wa miaka 35, alienda kuwaita majirani washuhudie kisa hicho nyumbani kwake lakini akatoroka, na polisi walikuwa wanaendelea kumtafuta.
Mke wake pia alitoroka baada ya kisa hicho.
Chifu wa eneo hilo Bw John Motobwa alisema Bw Gwaro aliwaambia wakazi kuwa bibi yake alikuwa anashiriki ngono na mwanamume mwingine jikoni mwa nyumba yake.
“Alimuumiza vibaya huyo mzee na kumwachia majeraha mabaya mwilini,” alisema Bw Motobwa.
Bw Chrisantus Asanyo ambaye ni mkazi wa eneo hilo alisema Bw Gwaro alikuwa amewaita kwake ili kushuhudia kisa hicho.
Walipofika katika nyumba hiyo ndipo walipompata Bw Omoke akiwa na maumivu makali, hajitambui, huku akilitamka jina la Vincent.
“Aliacha mkono ukiwa umekatwa na hapakuwa na dalili ya kuonekana kwa bibi yake hapo karibu. Bw Gwaro alitoroka baadaye,” alisema Bw Asanyo.
Aliongeza kuwa wawili hao walikuwa marafiki wa karibu sana na walikuwa wakifanya biashara pamoja. 
Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa Polisi katika eneo la Marani Bw Benjamin Kimwele alisema kisa hicho kilitendeka mwendo wa saa tatu usiku wa kuamkia jana.
Aidha, Bw Kimwele aliongeza kuwa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho na wanaendelea kuwasaka hao wawili ili kuandikisha taarifa.
Aliyejeruhiwa alipelekwa katika Hospitali ya Kimisheni ya Tenwek kwa matibabu zaidi.
“Mwathiriwa alikuwa na majeraha manne kwa kwa kichwa chake, shingo na mgongo,” alisema.
Mkuu huyo wa polisi aliwaonya wananchi dhidi ya kuchukua sheria kwa mikononi mwao, bali wawe wakipiga ripoti kwa polisi.
“Msichukue sheria mikononi mwenu wakati mizozo ya kinyumbani inapozuka. Muwaache polisi wafanye kazi yao ya kutatua uhalifu,” akasema Bw Kimwele.

from Blogger http://ift.tt/2kVtyOK
via IFTTT

Picha: Maelfu wajitokeza Kumzika Mchezaji Geofrey Bonny

Posted on

Maelfu ya wakazi Wa mkoa Wa mbeya wamejitokeza katika mazishi ya mchezaji Wa zamani Geoffrey bonny mwandanji aliyefariki dunia juzi na kuzikwa katika makaburi ya kanisa katoliki makandana wilayani Rungwe.

Wakizungumza wakati Wa mazishi baba mzazi Wa marehemu,bonifasi mashamba alisema amepokea kwa masikitiko kifo cha mwanae na kuongeza kuwa aliishi na watu vizuri jambo lililochangia watu wengi kujitokeza kumuuguza ikiwa ni pamoja na misaada mbali mbali.

Nae Mjomba Wa marehemu, innocent sigonda alisema marehem alikua akisumbuliwa na Kansas ya mapafu pamojs sukari ilikuwa ikishuka Mara kwa Mara.

Mwenyekiti Wa tawi LA yanga mkoa Wa mbeya alisema lusajo kifamba alisema marehemu alikuwa meanachama hivyo uongozi unasikitika kumpoteza mwanachama wake ambae alikuwa akitoa msaada Wa kiufundi kila alipotakiwa.

Naye mwakilishi Wa uongozi Wa yanga makao makuu shadrack nsajigwa alisema marehemu aliishi nae kama ndugu kwani walisaidiana na kupeana ushauri

Alisema marehemu alikua na kipaji cha Mpira pia alikua anajituma hivyo alikua mfano Wa kuigwa kwa vijsna waliopo

Aliongeza kuwa wachezaji Wa zamani no hazina kwa taifa hivyo ni vema wakatunzwa na kuthaminiwa aidha alitoa wito kwa wachezaji wengine kujipanga kimaisha ili baada ya kustafu wasisubiri kuomba misaada pindi wapatapo matatizo.

Alisema in vema pia kuanzisha vyama vya kuwasaidia kama wachezaji wastaafu.

Chanzo:Mbeya yetu

from Blogger http://ift.tt/2lvVM5z
via IFTTT

VIDEO ya Mama aliye fukua Kaburi la Mwanae Jijini Mbeya

Posted on

Tukio hilo limetokea mkoa wa Mbeya vijini Mbalizi katika tarafa ya utengule usongwe kitongoji cha Shigamba ambacho kipo barabara ya kwenda Unalike. Marehemu ni kijana mwenye umri wa miaka 22 na alifariki tarehe 16feb17 na kuzikwa tarehe hiyohiyo eneo na makaburini Shigamba barabara ya kwenda umalila. Isuzu wa kuamkia leo ikaonekana kaburi la kijana huyo limefukuliwa na Mama yake mzazi
Inasadikika na Mama yake mzazi akishirikiana na ndugu wa karibu kutokana na imani ya dini yao kwamba mwanae baada ya siku tatu atafufuka.baada ya kufukilwa walibeba
Mwili wa marehemu na kuupeleka nyumbani eneo la shigamba wakauosha na kuuvika suti wakisubiri siku tatu zifike ili aweze kufufuka Kama bwana wetu Yesu Kristu, Mwili wa marehemu umechukuliwa na polisi pamoja na Mama mzazi kwa uchunguzi zaidi.
ANGALIA VIDEO HAPO CHINI JINSI ILIVYOKUWA

from Blogger http://ift.tt/2m01jzk
via IFTTT

Mambo 5 yatakayo kusaidia mtu alie umizwa katika mahusiano

Posted on

Unapotaka kumshauri mtu aliyeathirika na mapenzi unatakiwa kuyafahamu mambo haya muhimu nayo ni:

1. Unatakiwa kujua maana ya upendo na gharama zake.

2. Lazima ujue vyanzo vya kujenga uhusiano ili uwe imara na mwenye nguvu katika maisha ya wapendanao.

3. Mambo 32 yanayojenga uhusiano kama ulivyosoma.

4. Lazima ujue mambo yanayoweza kuharibu mahusiano na milango ya kuvunja mahusiano.

5. Lazima ujue maumivu ya mapenzi ili uweze kuwaponya waliojeruhika kimapenzi.

from Blogger http://ift.tt/2lvO37G
via IFTTT

Fisi ajeruhi wanane Singida

Posted on

Singida. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba amesema watu wanane wameshambuliwa na fisi kati ya Februari 14 na 16.
Kutokana na hali hiyo, jana Magiligimba ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari na kutoa taarifa mapema pindi wawaonapo wanyama hao ili wadhibitiwe.
Amesema kuna baadhi ya familia zinazoishi kwenye nyumba maarufu tembe huweka milango imara ili kuwadhibiti fisi hao wasiingie ndani kirahisi.
Kamanda huyo ametoa wito pia kwa wanafunzi waendapo shuleni na wanaporejea jioni kuchukua tahadhari.
Amesema Februali 14, Ofisa Mendaji wa Mgongo, Mwajuma Lugamba (42)l alishambuliwa na fisi alipokuwa akirejea nyumbani akitokea kazini.
Amesema siku hiyo hiyo, watu wengine Masunga Ngusa (47) na Nkhamba Ngusa (27), walivamiwa na fisi walipokuwa wamelala kwenye nyumba yao ya tembe.
Wengine waliojeruhiwa ni Sunday Msengi (21) Faidda Ramadhan (9), Charles Juma (45),Yusuph Ally (22) na Ramadhan Juma (60)

from Blogger http://ift.tt/2kLSs2l
via IFTTT

Serikali yawasafirisha waliofukuzwa Msumbiji

Posted on

Mtwara. Baada ya Watanzania wanaoishi nchini Msumbiji kufanyiwa vitendo vya kikatili na kufukuzwa, Serikali mkoani hapa imelazimika kuwasafirisha kwa kutumia magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kuwafikisha karibu na mikoa wanakotokea.
Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama amesema hadi kufikia juzi, Watanzania waliojisajili katika mpaka wa Kilambo wakitokea Msumbiji walikuwa 220.
Amesema tayari watu 109 wa awamu ya kwanza wamesafirishwa, ambao waliishukuru Serikali na wakazi wa Mtwara kwa kuwapokea na kuwapa misaada mbalimbali.
Mmoja wa waliorudishwa, Mwajuma Abdallah amesema: “Tunawashukuru wanamtwara na Serikali kwa jumla kwa kutupokea vizuri leo (jana) tunarudi nyumbani.”

from Blogger http://ift.tt/2lvTaVj
via IFTTT

Viongozi watolewa hofu kuzungumzia njaa

Posted on

Shinyanga. Mbunge wa Shinyanga, Stephen Masele amewataka viongozi kuzungumza ukweli kuhusu njaa na kuacha kuogopa kutumbuliwa.
Masele amesema hayo jana wakati akitembelea kata mbalimbali za jimbo hilo ili kupokea kero za wananchi na kuzifanyia kazi.
Ameitaka Serikali kutambua kuwa wananchi wana njaa na hakuna chakula huku akiomba kilicjopo kuuzwa kwa kwa bei nafuu.
“Maeneo yote niliyopita nimekutana na vilio vya wananchi wakiomba msaada wa chakula kutokana na baadhi yao kudai wanakabiliwa na uhaba wa chakula na bei kubwa.
“Rais John Magufuli anaomba tumsaidie, na sisi tunamsaidia kwa kumwambia ukweli kuwa wananchi wana njaa watendaji wa Serikali hawasemi ukweli kwa hofu ya kutumbuliwa,” alisema Masele.

from Blogger http://ift.tt/2lZOxAJ
via IFTTT